Friday, July 26, 2013

0 comments
Je kwa nini obama anawakosesha mabinti zake masomo? Kila kona ya dunia anasafiri nao !

PAPA BENEDICT XVI, CHAMPIONI WAMABADILIKO

Saturday, July 6, 2013

0 comments

Papa Benedict XVI amejiuzulu. Sasa anaitwa Papa Emeritus Benedict XVI. Ni Papa bado, lakini si kwa muktadha wa kiutawala ndani ya viunga vya  kanisa la Mtakatifu Petro pale Vatikano. Kwa maana nyingine hana nafasi ya kimaamuzi kuhusu mwelekeo wa kanisa Katoliki Ulimwenguni.

Kwa vile katika wadhifa huu wa juu kiuongozi, hakuna kustaafu, twaweza kuwa sahihi zaidi kama tukisema kuwa Papa huyu amepumzika milele huku akimwachia Papa mpya wa mabadiliko Francis I, ili aweze kuhitimisha ngwe muhimu ya mabadiliko katika muktadha wa Omega.

Hili ni tukio kubwa sana ambalo ni nadra sana kutokea, na kwa  kuzingatia u-nadra huo ni vigumu tukio hilo, kuzoeleka  kiasi cha kulifanya lipoteze alama za nyayo zake katika mchanga wa historia ya sayari hii, dunia.

Ndio maana ulimwengu wote, kwa muda, umelazimika kupitia  ndani ya mawimbi ya bahari ya mtikisiko uliotokana na mtibuko uliosababishwa na tukio hilo. Kwa hikika mawimbi ya habari ya tukio hilo kuu yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza mwelekeo mpya wa kufikiri juu ya hatima ya dunia. Wakazi wengi wa dunia wanajiuliza kwamba; Je, Papa huyu mpya toka Province ya Argentina ana nini kibindoni kwa ajili ya dunia inayosusulika kiuchumi kisiasa na kimaadili?

Wakati huo-huo, baadhi ya wafuatiliaji wa karibu wa mchakato huu ambao hadi sasa tayari umeshazaa mipasuko ya ki-mtazamo na ki-maoni kuhusu kiini cha kujiuzulu kwake, wanaitafsiri sababu ya kujiuzulu huko ndani ya muktadha wa ombwe la kiutawala; kwamba Benedict ameshindwa kuhimili vishindo vya mikiki-mikiki ya changamoto za kiutawala kutokana na umri wake kumtupa mkono, na hivyo. Kama Papa mdhofu amejikuta akiishiwa na maono na weledi wa namna ya kuliendesha kanisa katoliki katika nyayo zenye mikito sahihi ya kimaamuzi.

Shadidisho la mlengo huo wa kimtazamo ni kauli iliyobubujika kutoka kinywani mwa muhusika mwenyewe; kwani aliweka wazi sababu iliyomsukumu kufanya uamuzi huo mzito. Kama mwanadamu nimepungukiwa nguvu kimwili na kiakili kuweza kumudu changamoto za kuliongoza kanisa wakati huu. Ni maneno yake mwenyewe hayo. Hakuyamung’nya wala hakuyatafuna.

Wako wanaotegemeza mikito yao ya ki-msimamo ndani ya muktadha huo-huo; lakini wakiongezea minofu na rojorojo za kimantiki kwa mbali ili kukikoleza kiini cha kujiuzulu kwake. Hawa, wanamchora Papa Emeritus katika taswira ya kiongozi shujaa na mbobevu ndani ya ulingo wa kitheolojia na  kidogma- mhafidhina, lakini, aliyeshindwa kumaliza mbio zake kwa ushindi mnono baada ya kuishiwa pumzi.

Kimsingi, wachunguzi wa kada hii wanajaribu kumchora Papa Emeritus kama kiongozi dhaifu kiutendaji, aliyeshindwa kuyasimamia maono yake mapevu na yenye ushawishi mkubwa. Naam, maono yaliyoisukuma koleji ya  makadinali kumweka kwenye kiti cha enzi pale Vatikano dhidi ya mpinzani wake wa karibu kadinali Bergoglio kwenye Conclave ya mwaka 2005.

Wadadavuzi wa kada hii hawaoni mwanga ng’ambo ya ushahidi uliopo wa mituhumiano ya kashifa, mdororo wa maadili,kutetereka kwa hali za kiroho ya waumini na skandali mbalimbali ndani na nje ya viunga vya Vatikano vilivyomjengea Papa Emeritus taswira ‘fifi’ ya Papa mshindwa, kwamba vikichunguzwa kwa tafakuri jadidi vyaweza kuwa kete ya kumjengea Papa huyu taswira mpya na ng’avu;  taswira itakayomweka ndani ya wingu la machampioni, kama mmoja wa mashujaa wa ki-mikakati aliyefanikiwa kulisimamia, kuliongoza na kulijenga kanisa katika ramani  tukuka ya ki-jesuiti. Naam, na hivyo kustahili pumziko la amani akimwachia kijiti Papa wa utaratibu Mpya wa Dunia, Francis I ili aweze kumalizia ngwe muhimu ya kuuleta ulimwengu pamoja.

Kwa kuzingatia ibuko, yaani, dokezo ng’ambo ya muktadha huo mfinyu wa taswira fifi ya Papa Emeritus, akili ya kawaida inashawishika kuzama ndani, vilindini, si kwa kubeza kauli yake binafsi aliyoitoa juu ya sababu ya kujiuzulu kwake. Kwa namna yoyote ile. Kauli hiyo yenye kuibua mitafunano ya hoja ilikuwa na munyu wenye ladha ya hekima. Kwani angetoa kauli gani kwenye muktadha kama huo bila kuibua minong’ono na mitafunano ya kalamu za waandishi mahili?

Labda niseme kuwa, kwa mujibu kauli zenye kuiweka wazi hekima ya makadinali, uteuzi wa mapapa wenye umri mkubwa ni mbinu ya kimikakati inayowasaidia wateuliwa kufanya mambo kwa kasi zaidi. Huepuka kutengeneza mazingira ya mbweteko wa mapapa ndani ya curia kutokana na mtaji wa umri, hivyo hulazimika kumbizana na umri wao.

Kwa maana nyingine, hata uteuzi wa Papa huyu mwenye damu ya kirumi toka Argentina, Francis, ambaye hadi sasa  umri wake ni  miaka 76 akimzidi mtangulizi wake kwa miaka miwili ya  kipindi cha uteuzi wake mwaka 2005, ni strateji ile-ile ya kuhakikisha kuwa jesuiti huyu naleta mtikisiko wa dunia; Na tayari Tumeanza kuona cheche zake.

Niseme kwamba, kama ilivyo kawaida ya binadamu aliyejizoeza kuzifikirisha akili zake, asiyepalilia na kurutubisha fikra bweteko, mweleke wa kifikra wenye kumtafsiri Papa Emeritus kama kiongozi mshindwa- mdhofu wa mwili na akili hauzimi kabisa kiu au muwashawasha wa kuzama ndani kabisa ya viunga vya Vatikano ili kuibuka na taswira mbadala, pengine, isiyo na ukungu, ili kuangaza juu ya muktadha halisi wa kujiuzulu kwake.

JFK 'S WARNING ABOUT SECRET SOCIETIES, nOW WE CAN CALL GLOBALISTS

2 comments

JFK tried to warn America about the “gnomes of Zurich,” but the elite killed him for his efforts. In his now famous “Secret Societies Speech,” JFK alerted American press and the American people of the perils faced by our people at the hands of what today we call the globalists. Below, are some selected quotes from his speech where he warned the country about the unfolding tyranny from the various secret societies. JFK’s words of over 50 years ago are more applicable today than they were at the time he spoke these words.
 “The very word “secrecy” is repugnant in a free and open society; and we are as a people inherently and historically opposed to secret societies, to secret oaths and to secret proceedings”
 

TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO

Thursday, July 4, 2013

1 comments

Makundi makuu matatu ya vidonda vya tumbo ambayo ni; vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula, yaani tumbo (gastric ulcers), vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers) na vidonda vinavyotokea kwenye koo (oesophageal ulcers).
Hata hivyo, wataalamu wanabainisha kuwa kuna aina kuu mbili tu zinazoathiri watu wengi duniani za ugonjwa huo. Hizi ni ile inayoathiri tumbo la kuhifadhi chakula (gastric ulcers) na ya pili ni ile inayoathiri utumbo mwembamba ujulikanao kama ‘duodenam’ ambao kwa kitaalamu hujulikana kama duodenal ulcers ambapo aina zote mbili kwa ujumla huitwa peptic ulcers.
 
Sababu za vidonda vya tumbo
Zipo sababu kadhaa za vidonda vya tumbo la chakula na utumbo mwembamba. Hapo zamani kulikuwa na dhana kwamba msongo wa mawazo (stress) na mlo (diet) husababisha vidonda vya tumbo.
Hata hivyo, baadaye watafiti wa masuala ya afya ya binadamu waligundua kuwa tindikali izalishwayo tumboni na vimeng’enya vya pepsini inachangia kiwango kikubwa katika kusababisha vidonda vya tumbo.
Lakini hivi karibuni utafiti umeonyesha kwamba zaidi ya asilimia themanini ya vidonda vya tumbo hutokana na bakteria aitwaye heliocobacter pylori (H.pylori). Aina hii ya vimelea vya bakteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 ya vidonda vya utumbo mwembamba (duodenal ulcers).
Vimelea vya H.pylori huweza kuishi kwenye ute ulindao tabaka la juu la tumbo na utumbo mpana. Hapo hutengeneza kimeng’enya kiitwacho urease ambacho hupunguza makali ya tindikali izalishwayo na tumbo, yaani gastric juice/acid. Ili kukabiliana na hali hii, tumbo hutengeneza tindikali nyingi zaidi ambayo huathiri tabaka la juu la utumbo.
Vimelea hivi pia hudhoofisha ute ulindao tabaka la juu la utumbo, hivyo kushindwa kulinda tumbo na utumbo mwembamba sawasawa.
Vimelea vya Hpylori huweza kusambaa kupitia chakula na maji. Vimelea vya bakteria hawa pia hupatikana kwenye mate, hivyo vyaweza kuambukizwa kupitia kinywa haswa iwapo mtu atabusiana na muathirika wa vimelea hivyo. Watu wengi pia huathirika na vimelea hivi utotoni.
Wataalamu wanabainisha kuwa matumizi ya dawa kwa muda mrefu ni moja ya sababu ya vidonda vya tumbo. Hii ufanya ukuta wa utumbo kujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo kwa kuwa na utando laini ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama prostaglandins.
Dawa huharibu mfumo wa kutengeneza vichocheo prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo husababisha kutokea kwa vidonda vya tumbo.
Uvutaji wa sigara: Kafeini na nicotine ambayo hupatikana kwenye baadhi ya vinywaji kama soda, kahawa pia kwenye sigara huchangamsha utengenezaji wa tindikali ya gastric tumboni ambayo huchubua ukuta wa utumbo na pia hutonesha kidonda kilichopo kama mtu ni mwathirika.
Ingawa inasadikika kwamba vigezo vyote hapo juu huchangia kupata vidonda vya tumbo, bakteria hpylori anasadikiwa kuwa chanzo kikuu katika kusababisha vidonda vya tumbo.
Aidha, wataalamu wanasema kuwa sababu za kijenetiki/vinasaba navyo ni moja ya kupata tatizo hilo la vidonda vya tumbo.

RAIS OBAMA: NA PROPAGANDA ZA KUTAWALA FIKRA ZA WASOMI WA KIAFRIKA

0 comments



Uko mkakati mzito unaoendelea chini kwa chini ili kuhakikisha kuwa  dunia yote inatweka vilindini mwa  mfumo wa kimaadili unaopwaya  siku si mbali tokea sasa. Kwa hakika huo ni mkakati  yakinifu unaoratibiwa kwa weledi mkubwa huku watu wenye misuli ya kimaamuzi wakishikilia mwelekeo mzima wa  ajenda hii tete na tata; Tutaangalia.

Wakati msukumo huo ukiendelea kutengeneza mwelekeo wa kimaadili ulio legelege, huku wale wote wanaojitahidi kusimama katika misingi kimaadili wakiwekwa fungu moja na kundi ya wahafidhina, watu waliathiriwa na misimamo ya kidogima isiyofungua wigo kwa mawazo mapya, kuna kila dalili zinazoonesha kuwa hatimaye dunia nzima, isipokuwa kundi la watu wachache, itapigishwa magoti chini ya bendera ya mfumo  wa kimaadili mdhofu utakaokuwa kama jeneza la mataifa tayari kwa mazishi.

Hatari iliyo kubwa zaidi, ni pale  hoja hizi momonyovu kimaadili zinapopenyezwa taratibu ndani ya mifumo ya kisheria huku zikiwa zimevikwa magwandwa yenye rangi  ya kidemokrasia na usawa kwa wote na hivyo kulichora kundi kinzani katika taswira fifi iliosheheni makengeza ya hitifaki ya usasa, unaoenzi misingi ya usawa na utu!

Mkakati huo unakwenda sambamba na upropagandisha uliokubuhu kwa hila, ili kutengeneza taswira isiyo sahihi kuhusu muktadha jumla wa dhana nzima ya neno maendeleo. Kwamba, wakati muktadha  uhusuo dhana ya maendeleo ya kweli wapaswa kumulikwa katika nyanja zote kwa ukamilifu wake, yaani; kiakili, kiafya, kimaadili na matumizi sahihi ya raslimali ndani ya kijamii husika, mataifa ya magharibi yanajaribu kujikita zaidi katika mtazamo finyu wa utajiri wa vitu; nyumba, magari, na vikorombwezo vyake, huku maeneo mengine muhimu hata kuzidi vikorombwezo hivyo yakiacha pembeni.

CONTACTS

0 comments
DR.JOSHUA LAWRENCE
TUMAINI JIPYA HERBATONIC CLINIC

SIMU
+255 753 333 003

EMAIL
drjoshualawrence@yahoo.com
drjoshualawrenceblog@gmail.com

SOCIAL NETWORKS

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

SEARCH IN THIS BLOG

JOIN ME ON FACEBOOK

BLOG FOLLOWERS

BLOG ACHIEVES

ADVERTISEMENT

ADVERTISEMENT

POPULAR NEWS

Je mtandao huu umekusaidia kujifunza na kupata maarifa Mapya...?